Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yakamilisha ratiba, DR Congo yafuzu hatua inayofuata

WhatsApp Image 2021 11 14 At 18.26.50.jpeg Stars yatoa sare na Madagascar

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars imepata sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Madagascar kwenye mchezo wa mwisho wa kundi J wa kuwania kufuzu kombe la Dunia.

Taifa stars imemaliza nafasi ya 3 kwenye kundi hilo, timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamemaliza vinara wa kundi.

Tanzania ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 25 kupitia kwa Simon Msuva, lakini kunako dakika ya 74 Hakim Abdallah akawasawazishia Madagar. Kwa matokeo haya Tanzania imefikisha alama 8, Madagascar alama 4.

Mchezo mwigine wa kundi J timu ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa nyumbani wameifunga Benini mabao 2-0, mabao ya Kongo yamefungwa na Dieumerci Mbokani na Ben Malango, Kongo wamefikisha alama 11, ndio vinara wa kundi na wamefuzu hatua ya mtoano inayofata, Benin wamemaliza nafasi ya pili na alama 10, Tanzania nafasi ya tatu na alama 8, na Madagascar wamemaliza na alama 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live