Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yakamilika

Stars Training Taifa Stars wanaendelea na mazoezi

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ujio wa nahodha Mbwana Samatta katika kikosi cha timu ya Taifa Tanzania unakamalisha orodha ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Mpaka jana katika mazoezi ya Stars upande wa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao waliwasili ni Simon Msuva na Novatus Dismas.

Samatta aliwasili nchini jana usiku na leo alikuwa akiiongoza Stars katika mazoezi yanayoendelea kwenye uwanja wa Mkapa.

Wachezaji waliopo katika kikosi cha Stars niĀ  Aishi Manula, Metacha Mnata, Ramadhan Kabwili, Shomari Kapombe, Israel Patrick, Kibwana Shomari, Edward Manyama, Mohamed Hussein na Erasto Nyoni.

Erasto Nyoni, Bakari Mwamnyeto, Lusajo Mwaikenda, Nickson Kibabage, Kennedy Juma, Meshack Abraham, Novatus Dismas, Mzamiru Yassin, Ramadhan Chombo, Zawadi Mauya na Feisal Salum.

Wengine ni John Bocco, Idd Seleman, Abdul Seleman, Mbwana Samatta, Kibu Denis, Reliants Lusajo na Simon Msuva.

MAJALIWA NDANI

Wakati mazoezi ya Stars yakiendelea Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliwasili na kwenda kutazama mazoezi hayo.

Majaliwa aliingia akiwa na maofisa usalama pamoja na kamati ya hamasa ya Stars na kwenda moja kwa moja uwanjani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz