Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yaichapa Niger ugenini, yatuma salamu Morocco

Charles M'mombwa.jpeg Stars yaichapa Niger ugenini, yatuma salamu Morocco

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Bao pekee la mchezo huo wa kwanza kuwania kufuzu Kombe la Dunia limefungwa na Charles M’mombwa dakika ya 60 akimalizia pasi ya Mbwana Sammata.

Ushindi huo unaifanya Stars kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi E ikiwa na pointi tatu nyuma ya Zambia ikiwa na utofauti wa mabao.

Kituo kinachofuata kwa Stars ni dhidi ya Morocco katika uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 21 saa 4:00 usiku

Chanzo: www.tanzaniaweb.live