Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yaanza vibaya majaribio

49f08cc8c2c4bfe49ba32985cdb8809e.jpeg Stars yaanza vibaya majaribio

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vibaya mechi zake za kirafiki dhidi ya wenzao wa Kenya, Harambee Stars baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi jana.

Timu hizo zitarudiana Alhamisi kwenye uwanja huo huo katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu.

Bao la kufuatia machozi la Taifa Stars liliwekwa kimiani na Ayub Lyanga katika dakika 37 baada ya Kenya kuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa katika dakika za awali.

Taifa Stars inajiandaa kwa mechi mbili za kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Gunea ya Ikweta utakaofanyika ugenini Machi 25 na ule wa nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Machi 30 dhidi ya Libya.

Tanzania iko katika Kundi J ikiwa na pointi nne wakati vinara Tunisia wana pointi 10 wakati Guinea ya Ikweta wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi sita na Libya wako mkiani kwa pointi tatu.

Tanzania inasaka kwa mara tatu kufuzu kucheza fainali za Afcon baada ya kucheza mara ya kwanza mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 Misri .

Kikosi cha Stars kilichoanza jana: Juma Kaseja, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Kelvin Yondani, Bakari Mwamnyeto, Hamid Mao, Idd Selemani, Feisal Salum, Farid Mussa, Salum Abubakar na Ayubu Lyanga.

Walioanzia benchi: Metacha Mnata,Yassin Mustapha Laurent Alfred, Dickson Job, Kelvin John, Abdul Hamisi na Deus Kaseke.

Chanzo: www.habarileo.co.tz