Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yaanza mazoezi, Kibu Dennis, Kibwana ndani

Training Stars Kikosi cha Taifa Stars kimeanza kufanya mazoezi leo Uwanja wa Mkapa

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Oktoba 4 kimeanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa ambapo zote zinapambana kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia wakiwa wapo kundi J.

Jonas Mkude hajaripoti kambini kutokana na matatizo ya kifamilia kwa mujibu wa Meneja wa Stars, Nadir Haroub,'Canavaro'.

Pia Shomari Kapombe naye jina lake awali lilitajwa ila kwa kuwa alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara alipokuwa akitimiza majukumu yake ndani ya Simba hajaripoti kambini.

Kocha Kim Poulsen ameonekana akiwapa program maalumu wachezaji wote ili kuwaweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

Kibu Denis na Kibwana Shomari ambaye amechukua nafasi ya Kapombe ni miongoni mwa wachezaji ambao wameripoti kambini leo na kuanza mazoezi Uwanja wa Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live