Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars matumaini kibao

8f054eba0251777e6747e3c569c2e360 Stars matumaini kibao

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ilitarajiwa kwenda Cameroon alfajiri ya leo kwa ajili ya kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) zinazotarajiwa kuanza kesho kutwa nchini Cameroon.

Stars inakwenda baada ya kujipima nguvu katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi DR Congo na kutoka sare ya bao 1-1, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Kocha Mkuu wa Stars, Ettiene Ndayiragije alisema kupitia mchezo huo ameona mengi ya kurekebisha ila kikosi chake kimeonesha matumaini ya kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

“Mechi kama hiyo tumeona mengi kuna mambo nilikuwa nawaambia wachezaji wangu hawaamini lakini wameona kuwa inawezekana tutafanyia kazi baadhi ya mapungufu yetu naamini tutakuwa vizuri,”alisema.

Alisema wanatengeneza kikosi cha vijana hivyo, uvumulivu unahitajika hasa pale wanapoona wamefanya makosa wawaache wazoee kwanza wanaweza kuja kuwa wachezaji wazuri wa taifa baadaye kama akina Aggrey Moris.

“Nawapongeza sana kwasababu hii mechi najua walikuwa na mchoko wa mwili nilijaribu kuwatia moyo ili waweze kuwa vizuri ndani ya dakika 90 kwa hiyo nimeona tunaweza kuwa na kitu kinachowezekana,”alisema.

Alisema iwapo watawaamini na kuwapa muda kuna timu kubwa huko mbeleni inakuja itakuwa bora zaidi. Kocha wa timu ya taifa ya DR Congo Florent Ibenge alisema Stars sio wabaya wanaweza kufanya vizuri na anafurahi kucheza nao na kumpa ushindani.

Alisema wanakwenda kwenye mashindano na bado ni vigumu kutabiri nani atakuwa mzuri hata Stars anaweza kuchukua ubingwa wa Afrika, kwani yale ni mashindano na kila mtu anataka kufanya vizuri.

Jumla ya wachezaji 30 waliitwa awali katika kikosi cha Stars kwa maandalizi ya fainali hizo kabla ya jana kuchujwa.

Wachezaji hao ni Aishi Manula, Juma Kaseja, Dan Mgore, Abdutwalib Mshery, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Edward Manyama, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Carlos Protas, Said Ndemla, Baraka Majogoro na Yusuph Mhilu. Wengine ni Ayoub Lyanga, Feisal Salum, Rajabu Athuman, Ditram Nchimbi, John Bocco, Deus Kaseke, Lucas Kikoti, Farid Mussa, Adam Adam, Dickson Job, Abdulrazack Hamza, Khelfinnie Salum, Samwel Jakson, Omari Omari na Paschal Gaudence.

Chanzo: habarileo.co.tz