Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars kuwafuata Wakenya jioni

69493 CHAN+PICHA

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha timu ya Taifa, Taifa Stars kinatarajia kuondoka nchini leo jioni kuwafuata Wakenya kwa mechi yao ya marudiano ya kuwania ushiriki wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) 2020 zitakazofanyikia Cameroon.

Stars iliyolazimishwa suluhu nyumbani wikiendi iliyopita, itaondoka jijini Dar saa 10 jioni kuwahi pambano hilo litakalopigwa jijini Nairobi, Jumapili hii.

Meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro' alisema maandalizi yapo vizuri na yeye anatangulia ili kwenda kuweka kila kitu sawa.

"Mimi nawahi kuondoka muda huu kwasababu kuna vitu natakiwa kwenda kuweka sawa, nazani mpaka saa kumi nao wataanza safari ya kuja," alisema.

Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka leo ni 20, huku mshambuliaji Ibrahim Ajib akiachwa kutokana na maumivu ya mguu yanayomkabili.

Katika mchezo huo Stars wanahitaji ushindi au sare ya magoli ndio waweze kuvuka kwenda hatua inayofuata, lakini kama wakitoka sare ya bila kufungana watapigiana mikwaju ya penalti.

Chanzo: mwananchi.co.tz