Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars kukipiga na Bulgaria leo

Vijana Stars Stars kukipiga na Bulgaria leo

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kikiwa chini ya makocha wazawa, Hemed Suleiman 'Morocco' na Juma Mgunda, jioni ya leo kitatupa karata ya kwanza kwenye michuano maalumu iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Fifa Series iliyoanza jana, wakati itakapovaana na Bulgaria.

Mechi inayochezwa kwenye Uwanja wa Dalga kuanzia saa 10:00 jioni ikiwa ni ya kwanza kwa Tanzania kwa miaka ya karibuni kuvaana na timu kutoka Ulaya, huku kocha Morocco alisema kikosi chote kipo fiti, tayari kwa pambano hilo kabla ya kurudi tena uwanjani Jumatatu kuvaana na Mongolia ya Asia.

Michuano hiyo mipya inashirikisha jumla ya nchi 24 za mabara sita tofauti zilizotengwa katika makundi sita yenye timu nne zitakazochezwa nchi za Algeria, Azerbaijan, Misri, Saudi Arabia na Sri Lanka.

Katika kundi la Azerbaijan lililopo Stars, kuna nchi za Mongolia, Bulgaria na wenyeji Azerbaijan ambao watashuka uwanjani usiku kuvaana na Mongolia katika pambano jingine la kitu hicho cha Baku.

Stars imefika salama Baku na kujifua tangu juzi, huku ikikutana na hali ya hewa na baridi kali, iliyoelezwa na kocha Morocco kwamba imemfanya wabadilishe aina ya mazoezi na kuahidi leo timu hiyo kupambana ili kupata ushindi mbele ya Bulgaria iliyocheza nusu fainali ya Kombe la Dunia 1994.

Katika fainali hiyo, timu hiyo ikiongozwa na nyota Hristo Stoichkov, aliyekuwa Mfungaji Bora wa fainali hizo zilizofanyika Marekani, Bulgaria ilimaliza ya nne kwa kufungwa 4-0 na Sweden katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.

Mbali na Stoichkov, Bulgaria imewahi kuwa na nyota waliotamba duniani akiwamo Dimitar Berbatov aliyewahi kuwika na Tottenham, Manchester United, Fulham za England na Monaco ya Ufaransa.

Akizungumzia maandalizi ya mechi hizo kocha Morocco, ambaye atamkosa nahodha, Mbwana Samatta, alisema licha ya hali ya hewa kuwa ngumu, lakini wamekomaa na mazoezi ili kuzoea hali hiyo kabla ya mechi hiyo ya leio na ile ya Jumatatu.

"Tupo vizuri na hatuna jinsi zaidi ya kujiandaa na mchezo huo katika hali ya hewa ya baridi ambayo ni ngumu kwa wachezaji, lakini kupitia mazoezi tuliyofanya tangu tufike hapa (Azerbaijan) wameanza kuizoea," alisema Morocco atakayewategemea Clement Mzize, Simon Msuva, Kibu Denis, Ben Starkie na Charles M'mombwa katika eneo la ushambuliaji.

Kikosi cha wachezaji 23 na makocha wapo kwenye msafara wa Stars unaoongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF), Dk Suleiman Jabir akiwa na Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live