Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars kuivaa Libya kwa Mkapa bila mashabiki

CS Constantine Sign Two Libya Internationals Zakaria Al Harish And Abdellah Al Arefi. Stars kuivaa Libya kwa Mkapa bila mashabiki

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mashabiki hawatopata fursa ya kuingia uwanjani kutazama mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) baina ya Taifa Stars na Libya utakaochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 29.

Hiyo inafuatia zuio la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kwa mechi hiyo na nyinginezo ikiwa ni hatua ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ingawa baadhi ya mechi zimepewa ruhusa ya kushuhudiwa na amshabiki viwanjani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya Caf, ni mechi 12 tu za raundi ya tano na ya sita ya hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Afcon ambazo zimepata ruhusa ya kuhudhuriwa na mashabiki huku kukiwa na zuio kwa mechi nyingine 30.

"Caf miezi na wiki chache zilizopita imewasiliana na wanachama wake wanaoshiriki Fainali za kuwania kufuzu fainali za Afcon huko Cameroon juu ya masuala ya protokali ya mechi, afya na miongozo ya kiusalamakwenye nchi zao.

Majadiliano hayo yamepelekea baadhi ya mechi kuwa kwa watu kuhudhuria chini ya usimamizi wa chama cha nchi kwa kufuata miongozo kutoka Caf na ile ya serikali katika nchi zao," alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa caf, Alexandre Siewe.

Mechi 12 pekee ambazo zimeruhusiw3a kuingiza mashabiki ni ule wa Mauritania na Morocco ambao mashabiki walioruhusiwa ni 900 tu, Burundi na Afrika ya Kati utakaohudhuriwa na mashabiki 5,000, Comoro na Togo ambao mashabiki walioruhusiwa ni 1000 kama ilivyo kwa mechi baina ya Sudan na Afrika Kusini.

Idadi ya mashabiki 200 tu ndio watakaoruhusiwa katika mechi sita ambazo ni ya Guinea ya Ikweta dhidi ya Tanzania, Niger dhidi ya Ivory Coast, Ethiopia na Madagascar, Burkina Faso na Sudan Kusini, Afrika ya Kati na Mauritania na ule wa Guinea Bissau dhidi ya Congo.

Nigeria yenyewe imeruhusiwa kuingiza 30% ya mashabiki katika mechi yake dhidi ya Lesotho na Madagascar yenyewe imeruhusiwa kuingiza mashabiki 1500 tu katika mechi yake nyumbani dhidi ya Niger.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz