Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars ijiandae vizuri kwa Afcon

E82d50b220acb98afc2c7fe5cd78d594 Stars ijiandae vizuri kwa Afcon

Sat, 13 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, iko kambini kujiandaa na mechi za kufuzu kwa fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2021 zitakazofanyika Cameroon mwakani.

Taifa Stars, ambayo iko katika Kundi J, itachezamechi mbili Machi 22 na 30 dhidi za Guinea ya Ikweta pamoja na Libya kwa ajili ya kusaka nafasi ya kwenda Cameroon katika fainali hizo.

Kabla ya kucheza mechi hizo mbili za Afcon, Taifa Stars itajipima ngubu mara mbili dhidi ya majirani zetu wa Kenya, Harambee Stars katika mechi zitakazofanyika Nairobi Machi 15 na 18 ili kuangalia uwezo wake kabla ya kuchezamechu hizo za kimashindano.

Kimsimamo, Taifa Stars wako katika nafasi ya tatu katika kundi lao wakiwa na alama nne baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoka sare mmoja na kufungwa mara mbili.

Timu inayoongoza katika kundi hilo ni Tunisia yenye pointi 10 ikifuatiwa na Guinea ya Ikweta yenye pointi sita na Libya ndio wanashika mkia wakiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi nne.

Kila kundi litatia timu mbili za kwanza ambazo zitafuzu kwa ajili ya fainali hizo, ambazo zitashirikisha jumla ya timu 24, ambazo zitapangwa katika makundi sita yenye timu nne kila moja.

Kutokana na utaratibu wa kufuzu kwa fainali, ambazo Tanzania ilishiriki kwa mara ya mwisho mwaka 2019 nchini Misri, Taifa Stars ina kibarua kigumu kuhakikkisha inafuzu kwani iko katika nafasi ya tatu wakati timu mbili ndizo zinatakiwa.

Mechi hizo mbili za majaribio ziwe na manufaa makubwa kwa timu yetu kwani inajulikana kuwa timu zetu na hata Taifa Stars huwa na tatizo kubwa katika ufungaji wa mabao.

Hivyo, ikiwa chini ya Kocha Mkuu mpya, Kim Poulsen, ambaye aliwahi kuifundisha timu hiyo huko nyuma, anatakiwakulifanyia kazi tatizo hilo ili kuhakikisha washambuliaji wetu wanafunga mabao ya kutosha na kupata ushindi.

Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishiriki fainali za Afcon mwaka 1980 na miaka 39 baadae ndio tukafanikiwa kufuzu kwa fainali hizo, hivyo tusitumie muda mrefu kukaa kando tukisubuiri kufuzu.

Libya na Guinea ya Ikweta sio timu mbovu, ila tunatakiwa kujipanga vizuri na kupambana kuhakikisha tunashinda mechi zetu na kufuzu jwa fainali hizo, ambazo awali zilitakiwa kuchezwa mwaka huu, lakini janga la Covid-19 likafanya isogezwe mbele.

Ni matarajio yetu kuwa Taifa Stars itafanya vizuri katika mechi hizo za majaribio na zile za kimashindano na kuiwezesha Tanzania kufuzu kwa mara ya tatu Afcon.

Mungu Ibariki Taifa Stas, Mungu Ibariki Tanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz