Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars, Tanzanite zawalaza Watanzania mapema, Maadhimisho miaka 60 ya Uhuru

Watoto Wa Kaguta Vikosi vya Timu za Taifa Stars na Tanzanite

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museven, wametia doa Sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.

Timu ya Taifa ya Uganda imeichapa Tanzania 2-0 usiku wa Alhamisi katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Uganda yamefungwa na Ivan Masaba dakika ya 71 na Joseph Bright dakika ya 90 wote wakimtungua kipa namba mbili nchini, Metacha Mnata wa Polisi Tanzania.

Katika vikosi vya timu zote mbili, vijana ndio hasa walioonekana kuchukua nafasi tofauti na majina yaliyozoeleka.

Wakati kipigo kikitolewa kwa Taifa Stars, Timu ya taifa ya wasichana ya Uganda imewafunga wenzao wa Tanzania 'Tanzanite' 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mapema majira ya saa 10 jioni.

Bao pekee la Uganda 'Created Cranes' limefungwa na Khadija Nandago dakika ya 18 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Janet Simba kufuatia mpira wa adhabu wa Samalie Nakacwa kutoka upande wa kulia baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Protasia Mbunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live