Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars, Tanzanite kuwapa Watanzania tabasamu la miaka 60 ya Uhuru leo

STARS UHURU Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini kabla ya mchezo

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Taifa Stars inataraji kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Crane’ saa 1:30 usiku wa leo Disemba 9, 2021 kwenye dimba la Mkapa kwa lengo la wanamichezo kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara.

Mchezo huohautohusisha wachezaji kutoka timu za Simba na Yanga kama ilivyozoeleka kutokana na timu hizo kuwa na ratiba ya kukutana kwenye mchezp wa Kariakoo Derby Disemba 11, 2021 kwenye dimba la Mpaka.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yussuph Singo amesema maandalizi yamekamilika hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi kwani kiingilio ni 2,000 tu

Kwa upande mwingine, Sherehe hizo pia zitaadhimishwa na wanasoka wanawake, ambapo timu ya taifa ya wanawake vijana chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ pia itacheza chini ya timu ya Uganda ya vijana saa 10:30 Jioni leo.

Kila tarehe 9 Disemba kila, Watanzania uungana popote walipo ili kusheherekea siku hiyo ambayo kwa sasa inajivunia kufanya mapinduzi makubwa ya kimaendeleo ikiwemo ya michezo yote kiujumla.

Chanzo: eatv.tv