Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stam kocha mpya Ken Gold

Stam Pic.png Amri Said 'Stam'

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

KEN Gold imethibitisha kumalizana na Amri Said 'Stam' kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya msimu ujao.

Timu hiyo ya wilayani Chunya inajiandaa na ligi ya Championship baada ya msimu uliopita kumaliza nafasi ya tano ikiwa chini ya Ngawina Ngawina aliyechukua nafasi ya Michael Mnyali na sasa inaanza kujipanga upya.

Stam anajiunga na timu hiyo ya wachimba dhahabu akitokea KVZ ya Zanzibar aliyomalizana nayo ligi kuu visiwani humo nafasi ya pili.

Nyota huyo wa zamani wa Simba aliwahi kuzifundisha timu kadhaa ikiwamo Msimbazi, Lipuli, Mbao, Mbeya City na sasa atakuwa na vijana hao kwa ajili ya msimu ujao.

Katibu mkuu wa Ken Gold, Benson Mkocha amesema baada ya kumalizana na benchi la ufundi sasa wanaeelekeza eneo la wachezaji na kuanzaia kesho Jumatatu wataanza kushusha mmoja baada ya mwingine.

"Stam amesaini mwaka mmoja na kuanzia kesho Jumatatu tutaanza kutangaza wachezaji kwa sababu mazungumzo yapo mwishoni, tunahutaji kupanda ligi kuu" amesema Mkocha.

Chanzo: Mwanaspoti