Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa Yanga awa raia wa Chuo

Salum Telela Staa wa Yanga awa raia wa Chuo

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Yanga SC, Salum Telela sasa ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika chuo kikuu cha Stella Maris Mtwara University college (STEMMUCSO) akisomea kitengo cha usimamizi wa Biashara (Business Administration)

Telela alisajiliwa na Yanga baada ya kung'aa kama beki wa kulia kwenye kikosi cha Serengeti Boys ingawa baadae alitumika zaidi kwa mafanikio kama kiungo wa kati kwa kipindi cha miaka 6 ya utumishi wake Young Africans SC.

Akiwa Yanga ameshinda mataji ya ligi kuu (2010/11, 2012/13, 2014/15, 2015/16,) kombe Kagame ( 2011 na 2012), Ngao ya Jamii (2013, 2014, 2015) na taji moja la FA.

Telela hajafanya makubwa sana akiwa uwanjani baada majeraha ya mara kwa mara lakini atakumbukwa kwa mechi zake mbili za CAF na 15 za VPL msimu wa 2014/15.

Magoli yake mawili bora zaidi kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Coastal Union na lingine dhidi ya Platnum FC bila kusahau ule mkwaju ulioipatia Yanga ubingwa wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC mnamo 2013.

Sio jambo rahisi kuacha soka na kuamua kurudi darasani tena akiwa na umri mdogo lakini Telela ambaye sasa ana umri wa miaka 30 sasa anapiga kitabu.

Telela anawakumbusha vijana kuwa inawezekana kuacha kazi ya taaluma/kipaji chako ikiwa maisha hayaendi na kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma ili kufikia malengo uliyojiwekea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live