Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa Soka apata ajali mbaya ya gari

Oscar Cardozo Staa wa Soka apata ajali mbaya ya gari

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Oscar Cardozo(39), amepata ajali ya gari baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kugonga Retro-Mercedez pamoja na nguzo ya taa huko Paraguay.

Kupitia mtandao wa Instagram Cardozo ameandika “ Kwanza kabisa naomba niwataarifu wote kuwa namshukuru Mungu niko salama na wahusika wengine wa ajali wapo salama pia, uliotokea ni uharibifu wa vifaa tu. Asanteni wote.”

Tukio hilo lilitokea Jumatatu jioni ikiwa ni chini ya masaa 24 tangu nyota huyo kufunga magoli manne katika kipindi cha kwanza cha mechi kati ya klabu anayoichezea ya Libertad dhidi ya Cerro Porteno. Mechi hiyo ilimalizika kwa matokeo ya 5-1.

Nyota huyo wa Paraguay aliwahi ´kuichezea Benfica kwa miaka 7 kati ya waka 2007 na 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live