Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa Brazil atengana na mkewe siku 24 baada ya kuoana

Adriano Adriano na Micaela

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasoka nguli wa Brazil Adriano ameripotiwa kutengana na mke wake, Micaela Mesquita.

Adriano na Micaela wanaripotiwa kuwa walifunga ndoa mapema Novemba ili kurasimisha uhusiano wao.

Kulingana na gazeti la The Sun, wapenzi hao walifanya harusi ya faragha na kushiriki picha zao walipokuwa wakitia saini karatasi rasmi za ndoa yao kwenye Instagram.

Lakini wiki tatu tu baada ya kufunga ndoa hiyo, ripoti nchini Brazili zinadai kuwa wapenzi hao wametengana. Tovuti ya habari ya Brazil Extra Globo inadai kwamba wanandoa hao wapya walitengana kufuatia ugomvi waliokuwa nao baada ya Adriano kuwatembelea marafiki zake huko Penha.

Mchezaji soka huyo wa zamani hakuwa pamoja na mke wake wakati wa ziara hiyo ya siku Tatu, iliyotokea usiku wa kuamkia mechi ya Kombe la Dunia ya Brazil dhidi ya Uswizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live