Winga wa Al Ahly Hussein El Shahat amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya pauni Laki Moja za Misri na mahakama ya Nasr kufuatia shambulio dhidi ya beki wa kulia wa Pyramids Mohammed El Chibi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu nchini Misri msimu uliopita.
Mahakama hiyo pia imemfungia nyota huyo Kwa miaka mitano kutojihusisha na shughuli yoyote ya kimichezo huku klabu ya Al Ahly nayo ikimpiga faini ya Pauni Laki 5 za Misri na kulaani kitendo hicho.
Chibi alilalamikia kudhalislishwa mbele ya umma wa waMisri, kupigwa na kutishiwa na winga huyo (31) na sasa ni hatihati kumuona tena El Shahat akicheza kabumbu.
Kumekuwa na Sheria Kali Kwa watu wanaopigana hadharani nchini Misri na tukio hilo licha ya Shahat kuhukumiwa adhabu kadhaa msimu uliopita bado nyota huyo hakuridhika na kushtaki mahakamani.