Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa Mamelodi augua ugonjwa wa akili, aokota makopo majalalani

Kessi Mdsf Khayelihle Shozi

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Khayelihle Shozi amezua taharuki baada ya kuonekana akiokota vyakula majalalani huku akidaiwa kuwa amepatwa na tatizo la ugonjwa wa akili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipitia Katika timu za vijana ya Mamelod Sundowns na kupandishwa hadi timu ya wakubwa, Baadaye alipelekwa kwa mkopo Katika Vilabu vya SuperSport United, Black Leopard, TS Galaxy na Richard Bays.

Khayelihle alipotea kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Oktoba 2021, na kutoweka bila kujulikana, alipokuwa akicheza na JDR Stars katika ligi daraja la pili Afrika Kusini.



Mnamo Januari 2022, alipatikana barabarani, akichimba kwenye mapipa ya takataka, na akiishi chini ya daraja.

Familia ya Shozi imesema haijakata tamaa katika kutafuta tiba ili kijana wao aweze kupona na kurejea katika hali yaje ya kawaida.

Msemaji wa familia, Simphiwe Shozi amesema kuwa jambo hilo limewaumiza kama familia kumuona mtoto wao akizagaa majalalani.

“Tumeshajaribu kila njia kumsaidia, hatuwezi kukata tamaa, inaumiza mioyo yetu kumuona mitaani hapa mjini, tunajaribu kadri ya uwezo wetu kumsaidia,” alisema Simphiwe.

Inaelezwa kuwa, mchezaji huyo alipelekwa kwa mshauri wa masuala ya kisaikolojia ili kumuweka sawa, lakini walipotaka kumrejesha kwa mara ya pili alitoroka. Shozi alipelekwa Sundowns mwaka 2010 na Mabhuti Khenyeza ambaye alikuwa akiichezea Chloorkop wakati huo.

Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Mamelodi, Pitso Mosimane ameonyesha kusikitishwa kwake na tukio hilo huku akielezea mchezaji huyo alivyokuwa muhimu kwenye kikosi chake wakati huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live