Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa KMC aendelea na matibabu

Staa KMC Mchezo wa KMC vs Coastal Union ulimalizika kwa KMC kushinda bao 1-0

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa kimataifa wa Tanzania ambaye ndiye mshambuliaji kiongozi wa Kinondoni Municipal Council KMC, Matheo Anthony ambaye alishindwa kuendelea na mchezo wa Ligi dhidi ya Coastal Union ya Tanga anaendelea na matibabu ambapo imeelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.

Matheo ambaye anaongoza kwa magoli 4 katika kikosi cha KMC FC alipata majeruhi baada ya kugongana na mchezaji wa Coastal Union hali iliyolazimu kukimbizwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu, hali yake inaendelea kuimarika.

“Mchezaji wetu Matheo baada ya kugongana na mchezaji wa Coastal na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu anaendelea vizuri”, alisema Ofisa Habari wa KMC Christina Mwagala.

KMC FC kufuatia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 bao la George Makang’a wameanza mazoezi ya kujiwinda na Polisi Tanzania mtanange utakaopigwa Disemba 22 dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live