Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa Arsenal aangua kilio kubaki kikosini

Mo Elneny Arsenal Mohamed Elneny

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari ndo hiyo. Staa Mohamed Elneny amefunguka na kudai kwamba ameangua kilio baada ya Arsenal kumsainisha dili jipya.

Mkataba wa awali wa mchezaji huyo wa Misri ulikuwa unafika tamati mwishoni mwa msimu uliopita, ambapo sehemu kubwa alikuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Baada ya kupata majeruhi ya goti Januari, Elneny alihojia kwamba maisha yake Arsenal yatakuwa yamefika mwisho. Lakini, mabosi wa Arsenal waliamua kumbakiza kwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja, jambo lililomfanya staa huyo aangue kilio. Alipofichua hilo, Elneny alisema: “Ilikuwa moja ya timu zangu za furaha kwenye maisha yangu.“

“Kwa namna walivyozungumza na mimi, kwa namna klabu ilivyofanya uamuzi, walinifanya nilie. Klabu ya Arsenal, inafahamu wazi ninavyoipenda kwa asilimia 100, naipenda sana.

Walijua sitaki kuondoka. Nilitaka kubaki na kumalizia maisha yangu ya soka nikiwa hapa. Nilikuwa majeruhi na mkataba wangu ulikuwa unafika wisho. Lakini, mkataba umekuja wakati nikiwa majeruhi.

Elneny ndiye mchezaji aliyeituimikia Arsenal kwa muda mrefu, alijiunga na timu hiyo Januari 2016, wakati ilipokuwa chini ya kocha Arsene Wenger.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live