Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ssetuba: Yule Chama anajua nyie

Ssetuba Ssetuba: Yule Chama anajua nyie

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

GOLIKIPA wa Biashara United, James Ssetuba, amekiri kushangazwa na uwezo wa hali ya juu wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama, hasa katika kutulia na mpira ndani ya boksi na kufunga kama alivyofanya pindi walipokutana juzi.

Ssetuba katika mchezo wa juzi dhidi ya Simba, alikubali kufungwa mabao matatu, Chama akifunga bao la tatu, kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kipa huyo alisema kuwa Chama ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji cha juu sana.

“Wapo wachezaji wachache sana wenye uwezo wa kutulia na mpira kama ambavyo alifanya Chama dhidi yetu, wengi huwa na papara kubwa wanapofika ndani ya boksi na mwisho wa siku huwa wanakosa mabao.

“Yeye alikuwa ni mtulivu sana na akafunga, kwetu kama safu ya ulinzi ya Biashara tumejifunza mengi na tunatakiwa kuwa makini katika michezo yetu ijayo hasa katika kuzuia kufungwa mabao kama yale,” alisema kipa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live