Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs yatakata England, yainyoosha Aston Villa

Skysports Son Heung Min Tottenham 5734572 Spurs yatakata England, yainyoosha Aston Villa

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Unai Emery jioni ya leo amekutana na kipigo cha aina yake akiwa nyumbani, wakati Tottenham Hotspur ilipoifumua Aston Villa kwa mabao 4-0 ikizidi kuifukuzia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.

Spurs imeipa kipigo hicho katika ushindi wa kuvutia uliopatikana kwenye Uwanja wa Villa Park, huku wenyeki wakicheza pungufu kutokana na John McGinn kupewa kadi nyekundu dakika ya 65 ya mchezo huo kwa kosa la kumchezea vibaya, Destiny Udogie.

James Maddison na Brennan Johnson walifunga mabao ya haraka kipindi cha pili muda mchache baada ya beki wa kati Micky van de Ven kulazimika kutoka nje kutokana na kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Radu Dragusin dakika ya 49 ya mchezo.

Maddison alifunga bao dakika ya 50 kabla ya Johson kuongeza la pili dakika tatu baadae na kuifanya Villa ianze kujipanga upya kusaka mabao ya kusawazisha, lakini dakika ya 65 ikajikuta ikicheza pungufu kwa kutolewa kwa McGinn na kuipa nafasi Spurs kutawala zaidi mchezo huo.

Katika dakika za majeruhi za pambano hilo, nahodha wa Spurs, Heung-min Son alifunga bao la tatu na Timo Werner akaongeza la nne na kukamilisha furaha kwa kocha Ange Postecoglou baada ya kulipa kisasi cha mabao 2-1 ilichopewa nyumbani msimu huu na wapinzani wao hao.

Kipigo hicho cha mabao 4-0 kwa Villa kimerejea kile cha Aprili, 2022 ilipofungwa idadi kama hiyo na kuhitimisha ubabe iliyowafanyia wapinzani wao kwenye mechi tatu mfululizo zilizopita za Ligi Kuu, ikishinda 2-0 kisha 2-1 katika mechi zilizofuata ikiwamo ya kwanza kwa msimu huu.

Matokeo hayo yameifanya Spurs kusalia nafasi ya tano ikiwa na pointi 53, ikiwa na mchezo mmoja wa kiporo, huku Villa ikisalia nafasi ya nne kwa alama 55 ilizonazo kupitia mechi 28.

Chanzo: Mwanaspoti