Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs yamkomalia Harry Kane

HARRY KANE M 1140x640 Spurs yamkomalia Harry Kane

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Tottenham wamempa Mshambuliaji wao, Harry Kane ofa mpya ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo kwa muda mrefu zaidi.

Inaelezwa Spurs ipo tayari kutoa mshahara wa zaidi ya Pauni 200,000 kwa juma, ambao anaupokea Kane kwa sasa ili kumshawishi asalie.

Katika siku za hivi karibuni wawakilishi wa Kane wanahusishwa kuwa kwenye mazungumzo na vigogo wa Ujerumani FC Bayern Munich, ambao wanaitamani huduma ya fundi huyu.

Mahrez atengewa mshahara mnono Saudi Arabia Kocha wa Munich, Thomas Tuchel anadaiwa kumpigia simu Kane ili kumshawishi akubali kujiunga na timu yake katika dirisha hili.

Kane mwenye umri wa miaka 29 mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao na hadi sasa bado hajafanya uamuzi ikiwa anataka kuondoka ama kubaki.

Msimu huu amecheza mechi 49 za michuano yote na kufunga jumla ya mabao 32.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: