Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs yakubali kumuuza Cristian Romero

Cristian Romero Cristian Romero

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tottenham haina mpango wa kukubali ofa yoyote kutoka kwa Real Madrid au timu nyingine inayohitaji saini ya beki wao raia wa Argentina Cristian Romero, 26, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Romero mwenye umri wa miaka 26, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 35 za michuano yote.

JUVENTUS inataka kumtumia mshambuliaji wao raia wa Italia, Federico Chiesa, 26, kama sehemu ya ofa itakayoituma kwenda Manchester United kwa ajili ya kumsajili Mason Greenwood katika dirisha hili.

Greenwood mwenye umri wa miaka 22, amekuwa katika rada za timu kibao barani Ulaya zilizovutiwa na kiwango alichoonyesha msimu uliopita akiwa na Getafe.

MSHAMBULIAJI wa Paris St-Germain na Uholanzi Xavi Simons ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo RB Leipzig amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anataka kuondoka mwisho wa msimu huu aidha kwa kutolewa kwa mkopo ama kuuzwa mazima.

Bayern Munich ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili. Mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

MPANGO wa Leeds wa kutaka kuipata saini ya beki wa Tottenham Joe Rodon katika dirisha hili huenda ukafeli baada ya staa huyo kuonyesha uhitaji wa kutaka kujiunga na timu inayoshiriki Ligi Kuu England ambapo Leicester, Ipswich na Southampton zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Mkataba wa fundi huyu unamalizika mwaka 2026.

AC Milan imejiondoa katika mchakato wa kumsajili straika wa Bologna, Joshua Zirkzee, ambaye ilihitaji kumsajili katika dirisha hili na hiyo inaipa nguvu Manchester United kufanikisha mchakato wa kumpata kwa sababu Milan ndio ilikuwa mpinzani wao wa karibu katika dili hilo.

Milan imehamia kwa Tammy Abraham ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

KWA mujibu wa gazeti la Sunday Mirror, Liverpool imefanya mawasiliano na Juventus ili kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo na Italia Adrien Rabiot, katika dirisha hili. Liverpool inataka kuboresha eneo lao la kiungo ambalo halikuwa na uwiano mzuri msimu uliopita.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2024. Msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote.

BRIGHTON imeonyesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Galatasaray na Uturuki, Baris Alper Yilmaz, 24, katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha kwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi 57 za michuano yote, amefunga mabao sana na kutoa asisti 12.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Chanzo: Mwanaspoti