Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs yaichapa Arsenal, Vita ya Top Four haishikiki

Kane Scoring Mshambuliaji wa Spurs Harry Kane akishangilia moja ya magoli yake usiku wa jana

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wa Antonio Conte, Tottenham Hotspur wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.

Mabao ya Spurs yamefungwa na Harry Kane mawili, dakika ya 22 kwa penalti na 37 akimalizia pasi ya Rodrigo Bentancur na lingine Son Heung-Min dakika ya 47.

Kwa ushindi huo, Spurs inafikisha pointi 65, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa pointi moja moja na Arsenal baada wa wote kucheza mechi 36.

Arsenal ilimaliza pungufu baada ya Rob Holding kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 33 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live