Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs wakamilisha usajili wa Radu Dragusin

Radu Dragusin Is Next On Tottenham Transfer Radar beki Radu Dragusin

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tottenham Hotspur imefikia makubaliano ya kumsajili beki Radu Dragusin kutoka klabu ya Genoa na kumaliza sakata la nyota huyo ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Bayern Munich.

Sky Italia inaripoti kwamba Bayern Munich ilijaribu kuizidi kete Spurs dakika za mwisho lakini nyota huyo raia wa Romania aliamua kuheshimu makubaliano ya awali na miamba hiyo ya London na kuwabwaga vigogo hao wa Ujerumani.

Spurs italipa kitita cha zaidi ya euro milioni 30 pamoja na beki Spence ambaye atapelekwa upande wa pili kwa mkopo. Dragusin (21) atasafiri kuelekea London Leo kwa ajili ya kukamilisha usajili huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live