Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs kutema wachezaji tisa

Lucas Moura Spurs Lucas Moura

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Tottenham Hotspurs imetangaza itawatema wachezaji tisa katika dirisha hili la usajili la kiangazi, baaada ya mikataba yao kumalizika mwisho wa mwezi huu.

Mabadiliko hayo ni kutokana na kocha mpya Ange Postecoglou aliyeteuliwa hivi karibuni kwasababu ana mipango yake kuelekea msimu mpya wa 2023-2024.

Taarifa iliripoti kupitia tovuti ya klabu yao, Clement Lenglet anatarajia kurejea Barcelona baada ya mkopo wake kumalizika.

Mchezaji mwingine anayeondoka baada ya mkopo kumalizika ni Arnaut Danjuma na atarejea Bournemouth.

Danjuma alicheza mechi 12 akiwa na uzi wa Tottenham msimu uliopita na akafunga mabao mawili.

Tayari klabu hiyo ilitangaza Lucas Moura, ambaye alifunga mabao 39 goals katika mechi 221 ataondoka msimu ukimalizika.

Mwingine ambaye yupo njiani kutimka ni Fagan Walcott licha ya kujumuishwa kikosi cha kwanza msimu uliopita, ikumbukwe beki huyo alianza kuonekana katika mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya, Spurs ilipocheza dhidi ya RB Leipzig mwaka 2020.

Jamie Bowden na wachezaji wengine vijana wenye umri wa miaka 18, Thomas Bloxham, Brandon Bryan-Waugh and Riley Owen watatemwa na klabu hiyo hivi karibuni.

Tottenham imepanga kufanya usajili wa kwanza chini ya kocha mpya Postecoglou, tayari mchezaji kutoka Leicester City, James Maddison amehusishwa lakini bado hawajuma ofa.

Chanzo: Mwanaspoti