Liverpool imegawana alama na Tottenham Hotspur kwa kutoa sare ya goli 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa dimba la Spurs ikishuhudiwa Andrew Robertson akionyeshwa kadi nyekundu.
Tottenham walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji Harry Kane ambaye alifunga goli la kwanza msimu huu akimalizia pasi ya Tanguy Ndombele katika dimba la nyumbani, bao ambalo lilisawazishwa na Diogo Jota muda mfupi kabla ya mapumziko akimalizia krosi wa Robertson.
Ungwe ya pili, Robertson aliipa Liverpool uongozi ingawa ndani ya muda mfupi waliweza kuruhusu goli lingine kupitia kwa nyota wa Korea Kusini Son Heung-min.
Sare hiyo inamaanisha kuwa Liverpool imepoteza nafasi ya kusherekea sikukuu ya christmas wakiwa hawaongozi msimamo wa EPL, mara ya mwisho kutoongoza ilikuwa miaka minne iliyopita.
Sasa kocha Antonio Conte anafikisha mechi ya tano nila kupoteza.