Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Sports Countdown' ya EA Radio leo Agosti 24

Chama La Yangaaaa Kikosi cha Yanga kikiwa Mazoezini nchini Morocco Kabla ya Kambi hiyo Kusitishwa

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Simba na Yanga kurejea nchini leo zikitokea nchini Morocco kwenye kambi zao ili kujiunga na kambi ya timu ya taifa keshop Agosti 25, 2021. 'Sports Countdown' Ya EA Radio inakupitisha kuzihesabu zile stori sita kali za michezo leo Agosti 24, 2021.

6 – Ni idadi ya siku ambazo klabu ya Yanga imefanya mazoezi kamili kwenye kambi yake waliyoweka kwenye mji wa sale nchini Morocco kujiandaa na michezo ya hatua ya awali ya mtoano kuwania kufuzu makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika na mashindano mengine ikiwemo ligi kuu bara.

Kambi hiyo imesitishwa rasmi hapo jana kwa kile kilichotajwa ni kutokana na sababu mbalimbali kwa maslahi mapana ya klabu hiyo huku ikiaminika watawasili nchini leo Agosti 24, 2021 na wachezaji wake wengine watano watajumuika kwenye kambi la timu ya taifa itakayoanza kesho Agosti 25, 2021.

5 – Ni idadi ya magoli yaliyofungwa usiku wa hapo jana kwenye mchezo mmoja wa EPL uliochezwa kati ya Westham United na Leicester City uliomalizika kwa Westham United kupata ushindi wa mabao 4-1 sawa na kuwadondoshea kitu kizito kichwani Mbweha hao wa England na kushika usukani wa ligi wakiwa na alama 6 sawa na Chelsea na Liverpool.

Mabao ya Westham yamefungwa na Pablo Fornals, Said Benrahma, Michail Antonio akufunga mawili na Yuri Tielemans akifunga moja la kufutia machozi kwa Leicester City. Mabao mawili ya Michail Antonio yanamfanya afikishe idadi ya mabao 48 na kuivunja rekodi ya Paolo Di Canio aliyefunga mabao 47 na kumfanya Antonio kuwa mfungaji wa muda wote Westham United.

4 – Ni idadi ya miaka aliyosaini mlinzi wa kulia wa klabu ya Bayern Munich, Joshua Kimmich kuendelea kusalia klabuni hapo hadi mwaka 2025. Kimmich ambaye anauwezo wa kucheza nafasi ya kiungo amesema ameendelea kusalia na miamba hiyo baada ya kuvutiwa na project yao ya kutaka kuendelea kushinda mataji na kutawala barani ulaya.

Ikumbukwe kuwa, Kimmich ni mshindi wa kombe la michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu wa mwaka 2019-2020 akiwa na Bayern Munich pamoja na kutwaa makombe 6 mfululizo ya Germany Bundesliga na kombe la Dunia la vilabu pamoja na kucheza michezo 260 na kufunga mabao 30.

3 – Ni miaka ambayo kiungo kiungo Cleatus Chota Chama aliitumikia klabu ya Simba ya Tanzania kabla ya hapo jana kuthibitishwa rasmi kujiunga na klabu yake mpya ya RS Berkane ya nchini  Morocco kwa kusaini kandarasi ya miaka mitatu.

Chama atasalia kuwa kwenye mioyo ya Wanasimba baada ya kuwakonga nyonyo kwa kusakata kandanda safi lililomfanya aitwe 'Mwamba wa Lusaka' au 'Mzee wa Locomotive fent' na kushiriki kwenye mafanikio makubwa ya kihistoria ya klabu hiyo ya kusaidia kutinga hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika mara mbili ndani misimu mitatu, kushinda VPL mara tatu mfululizo na makombe mawili ya TFF Azam Sportss federation Cup.

2 – Ni nafasi aliyokuwa anashikilia Andy Murray kwenye viwango vya ubora kwa miaka iliyopita ambapo nyota huyo raia wa England amefanikiwa kutinga hatua ya mzunguko wa pili ya Mashindano ya Wiston Salem Open inayofanyika nchini Marekani baada ya kumfunga Noah Rubin usiku wa kuamkia leo.

Murray alilazimika kucheza na Noah baada ya mshindani wake Nick Kyrgois wa Autralia kupata majeraha ya goti. Ushindia seti 6-2 na 6-0 unamfanya Andy Murray kutinga hatua ya mzunguko wapili kucheza dhidi ya Mmarekani Frances Tiafoe.

1 – Ni idadi ya mwaka ambao nyota wa zamani Philadelphia 76ers Josh Richardson ameongeza kuendelea kuitumikia timu ya Boston Celtics kwenye msimu mpya wa NBA unaotaraji kuanza Oktoba 19, 2021 na kumalizika Aprili 10, 2021.

Richardson anataraji kuwa sehemu ya michezo mitano mahususi ya NBA kuadhimisha miaka 75 tokea kuanzishwa kwake michezo ambayo itaanza mwezi Novemba na kumalizika mwezi Januari. Michezo hiyo ni Toronto Ratptors dhidi ya New York Knicks ukiwa ni kumbukizi ya kihistoria ya mchezo wa kwanza wa NBA mwaka 1946, Golden State Warriors na Boston Celtics, Golden State Warrirors dhidi ya New York Knikcs ilhali Los Angeles Lakers watacheza na Atlanta Hawks kwa upekee wa rekodi ya kibabe ya Lakers kuifunga mara 33 ikiwa ni mara nyingi zaidi kwa mpinzani mmoja tena michezo 33 mfululizo.

Chanzo: eatv.tv