Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Sports Countdown' ya EA Radio Agosti 31

Cristiano Ronaldoo Cristiano Ronaldo

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

6 - Ni muda ambao dirisha kubwa la usajili nchini England litafungwa usiku wa kuamkia kesho Septemba 1, 2021 baada ya kufunguliwa kwa takribani kwa miezi miwili kuruhusu vilabu kusajili wachezaji wanaowahitaji ili kuimarisha vikosi vyao.

Dili la mshambuliaji kinda, Kylian Mbappe kutoka PSG kwenda Real Madrid huenda likabuma baada ya PSG kushindwa kujibu ofa ya Real Madrid ya paundi milioni 170 sawa na zaidi ya bilioni 510 za kitanzania ili kumsajili mkali huyo wa kufumania nyavu.

Kwa upande mwingine, klabu ya Wolves ya England ipo kwenye mazungumzo na Lille ya Ufaransa ili kumsajili kiungo Renato Sanchez.

5 - Ni idadi ya makombe ya ligi kuu nchini Ukraine aliyoshinda mchezaji Willian alipokuwa anaichezea klabu hiyo miaka 8 iliyopita klabu ya Kujiunga na Chelsea 2013 na kutimkia Arsenal 2020.

Winga huyo ambaye anasifika kwa kuwa na kasi sana mithili ya kibelenge amesitisha mkataba wake wa miaka miwili na Arsenal kwa kulipa gharama za paundi milioni 20 za England sawa na bilioni 60 za kitanzania na kuhamia klabu yake ya zamani ya Corinthians ya nchini kwao Brazil huku akikubali kukatwa asilimia 70 ya mshahara wake wa paundi 248,000 za England sawa na milioni 740 za Kitanzania.

Willian anaondoka Arsenal akiwa amecheza michezo 37 kwenye michuano yote, akitoa assit 7 na kufunga bao 1 pekee na kutwaa ngao ya hisani ya Jamii 2020 baada ya Arsenal kuwafunga Manchester City.

4 - Ni idadi ya makundi maalum yanayotakiwa kupata chanjo ili waruhusiwe kushiriki ligi kuu ya kikapu nchini Marekani NBA kwa msimu ujao unaotaraji kuanza October 19 na kutamatika April 10, 2022.

Makundi hayo ni kundi la Wachezaji, Makocha, Wafanyakazi wasaidizi wa uwanjani pamoja na waamuzi wa ligi hiyo. Suala la chanjo limetolewa kama Agizo kutoka wasimamizi wa NBA kwa kusema wamejali afya za watu kujikinga na Covid-19.

3 - Ni idadi ya makombe ya EPL ambayo CR7 ameyashinda mara 3 mfululizo mwaka 2007, 2008 & 2009 akiwa na Manchester United tokea 2003 na kabla ya kuhamia Real Madrid mwaka 2009.

Cr7 atarejea kwenye klabu yake hiyo baada ya usiku wa jana Manchester United kuthibitisha kukamilisha usajili wa mchezaji huyo kwa ada ya uhamisho wa paundi 20mil sawa na bilioni 60 za Kitanzania kutoka Juventus ya Italia na kusaini kandarasi ya miaka miwili yenye kipengele cha kuongoza cha kurefusha mwaka mmoja.

CR7 anatazakiwa kulipwa paundi 480,000 za England sawa na bilioni 1 na zaidi ya milioni 400 na kumfanya awe mchezaji anyelipwa mshahara mnono kuliko wote EPL kwasasa.

2 - Ni miaka miwili imepita tokea Johanna Konta atinge robo fainali ya michuano ya wazi ya tennis, US Open inayofanyikaga nchini Marekani.

Konta ambaye anashika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora mchini England na wa 47 kwenye viwango vya ubora duniani kwa wacheza tennisi amejiondoa kwenye mashindano hayo yaliyoanza jana ikiwa ni muda mchache kabla hajacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Mfaransa Kristina Mladenovic huku chanzo cha kujitoa kwake ikielezwa na maumivu ya goti yaliyokiwa yanamsumbua kwa muda mrefu.

Ikumbukwe kuwa Johanna Konta aliikosa michuano ya Wimbledon baada ya kuwa karibu na mwenye COVID-19 na baadae kuikosa michuano ya TOKYO OLYMPIC baada ya kupata Covid-19. Hakika huu ni mwaka wa shetani kwa Konta.

Kwa upande wa tennis ya wanaume, Andy Murray anayeshikilia nafasi ya 114 kwa viwango vya ubora duniani kwasasa ametolewa kwenye hatua ya mwanzoni baada ya kufungwa seti 2-6, 6-3, 6-3, 3-6 & 6-4 na Mgiriki Stefanos Tsitsipas anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza hatua ya 64 bora usiku wa kuamkia leo na Tsitsipas sasa atacheza na Adriano Mannarinon raia wa Ufaransa anayeshikilia nafasi ya 44 kwa ubora duniani kwenye hatua ya 32 bora saa 12:00 jioni ya leo.

1 - Ni siku iyobaki ili dirisha kubwa la usajili kwa msimu wa mwaka 2021-2022 lifungwe kwa vilabu vya Ligi Kuu, Championship, First league na Ligi kuu ya Wanawake. TFF inavitaka vilabu vihahikishe vina kamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa maana hatutakuwa na muda wa ziada.

Wakati dirisha hilo likitazamiwa kufungwa saa sita usiku wa leo Agosti 31,2021 Mshambuliaji Adam Adam amejiunga na Polisi TZ kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Alwahda ya Falme za kiarabu, Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mohamed Rashid amejiunga na Mbeya Kwanza wakati ambao tetesi zinaeleza Abdi Banda atajiunga na Mtibwa Sukari akitokea Afrika ya Kusini na Mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage atajiunga na KMC kutokea Youssoufia ya Nchini Morocco.

Chanzo: eatv.tv