Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SportPesa yafunguka kumalizika kwa mkataba wao na Simba, Yanga

Tarimba 1 Tarimba Abbas

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Mikataba wa Mdhamini Mkuu wa Klabu pendwa zaidi nchini nambao pia ni Watani wa Jadi, Simba SC na Yanga SC ikiwa inakaribia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas ametolea ufafanuzi jambo hilo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari waliotaka kujua hatma ya mazungumzo yao na miamba hiyo ya soka Afrika Mashariki na Kati.

”Ikifika mwishoni mwa msimu huu, inamaana mikataba yetu itakuwa imeshatimiza miaka mitano. Sisi tumeshazungumza na Simba SC kuonyesha kwamba tunataka kuendelea kudhamini Simba Sc.

"Vvilevile tunaongea na Young Africans Sports Club kuhakikisha kuwa tunaendelea na mkataba huu,” amesema Tarimba.

Ikumbukwe kuwa, Muwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Mohammed Dewji aliwahi kudai kwamba, Simba haipati hata asilimia moja ya kiasi cha fedha kutokana na mkataba wa udhamini wa jezi ‘shirt’ wa SportPesa huku akiitolea mfano Manchester United kwa kitita inachokiingiza kutokana na mkataba wa udhamini wao.

”Manchester United has agreed to a $305 million shirt sponsorship contract for 5 years. @SimbaSCTanzania doesn’t get even 1% of that with sports Pesa. Time has come to look out for better pastures,” aliandika Dewji.

Aidha, Mo Dewji aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema Simba ni Klabu kubwa, ina mashabiki wengi, imewekeza pesa nyingi na mafanikio makubwa kwa miaka minne, hivyo sio fair kuipa kiasi sawa cha mkataba sawa na vilabu vingine vya ligi hapa nchini.

"Kwa utafiti tuliofanya, mashabiki wa Simba nchini ni 67%-70%, purchasing power yao ni kubwa zaidi, hivyo SportPesa wana-bid zaidi, tumepoata vikombe vinnne vya Ligi, Shirikisho viwili, Simba Queen mbili, Ligi ya Mabingwa Robo Fainali, tuko nafasi ya 12 wenzetu 88," alisema Mo Dewji.

Simba SC na Yanga SC ziliingia kandarasi ya miaka mitano na Kampuni SportPesa mwezi Mei, 2017.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live