Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika aagiza Tembo Warriors wapelekwe bungeni

46e9caf8c2366e90c350001fe025ca45 Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameagiza timu ya soka ya Taifa ya watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’, ipelekwe bungeni kesho kupongezwa kwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Ametoa kauli hiyo leo, baada ya kanuni za bunge kutenguliwa na kuruhusu timu ya soka Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Girls’ kuingia ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.

Serengeti Girls imepewa heshima hiyo ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwapongeza kwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika India Oktoba mwaka huu.

Spika alisema kwa vile Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, amesema Tembo Warriors imefuzu fainali za Kombe la Dunia, hivyo nayo ipelekwe bungeni.

“Naagiza Tembo Warriors nao waletwe bungeni kesho,” amesema Spika Tulia na kushangiliwa na wabunge.

Chanzo: www.habarileo.co.tz