Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spalletti: Sidanganyiki na kiwango cha Liverpool

Luciano Spaletti Kocha mkuu wa Napoli Luciano Spalletti

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Napoli, Luciano Spalletti amesema Napoli “haitadanganywa” na matokeo ya hivi karibuni ya Liverpool wala Jurgen Klopp hawawezi kupata ushindi hii leo mbele yao kwenye Kundi hilo A kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kikosi cha Klopp kama kinataka kuongoza kundi hilo lazima kiwashinde Napoli kwa mabao saba hapo Anfield siku ya leo baada ya kuchapwa 4-1 na Napoli siku ya kwanza ya mechi wakiwa ugenini na baadae wakashinda mechi zao zote.

Wakati Liverpool wakitinga hatua ya mtoano wakiwa wamebakiza mechi moja, Majogoo hao wa Anfield wametetereka katika Ligi kuu England msimu huu wakiwa wamekaa nafasi ya tisa kwenye msimamo huku wakiwa nyuma pointi 15 dhidi ya kinara Arsenal.

Klopp amesema kuwa ushindi wa mabao hayo hautawezekana kutokana na uwezo ambao walionao Napoli ambao wanashiriki Serie A, huku akiitabiria timu hiyo kutinga fainali ya michauno hiyo, lakini Spalletti akipokea taarifa hizo kama zimetiwa chumvi.

Spalletti amesema; “Nadhani nimesoma kwamba alisema hawafikirii kushinda 4-0 nadhani alisema hivyo kwa uzito, Kama alisema kwa dhati kwamba hawezi kushinda hayo mabao, akitaka tuzungumze basi Pongezi nyingi wakati mwingine hutumika kukuinua na kukuangusha”.

Spalletti aliendelea kusema kuwa Klopp ametinga fainali mbili za mwisho za Ligi ya Mabingwa, hivyo ni bora kuliko kila mtu, yeye na timu yake. Tunakubali pongezi ikiwa ni za dhati, lakini pongezi hazileti matokeo na msimamo.

Mchezo utakuwa mgumu sana na wanalazimika kuwa sawa na kawaida kama katika mechi ya kwanza na ni vigumu kurudia mechi hiyo. Ili kumaliza wa kwanza au wa pili kila kitu kinabadilika na inakuwa haipendezi kujibu swali la tunataka kushinda au la.

Kocha huyo anasisitiza kuwa anaiona Liverpool sawa tu na siku zote na hawadanganyiki na kuwa imekuwa na matatizo hivi karibuni, lakini pia alivitaja vilabu kama Manchester City, Chelsea kuwa wana wachezaji bora Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live