Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Southgate yupo sana England, FA wafunguka

Gareth Southgatee Kocha wa England, Gareth Southgate

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gareth Southgate ataendelea kubakia katika majukumu ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England mpaka mashindano ya Euro 2024.

Taarifa za kubakia kwa mchezaji huyo wa zamani katika nafasi ya ulinzi ya England zimethibitishwa na Chama cha Soka ambacho kimesema yeye (Southgate) na kocha wake msaidizi wataendelea kusalia kwenye nafasi zao mpaka 2024.

Southgate, 52, alikuwa kwenye mjadala wa iwapo atasalia au ataondoka kutokana na timu ya taifa ya England kuishia hatua ya robo fainali wakitolewa na Ufaransa lakini kwa taarifa ya FA ni kuwa sasa ‘mwamba’ ataendelea kuwanoa Three Lions.

“Tunafuraha kuwaambia kuwa Southgate ataendelea na majukumu yake mpaka Euro 2024”, alisema Mtendaji Mkuu wa FA, Mark Bullingham.

Southgate aliteuliwa rasmi kuwa kocha wa England mwaka 2016 akichukua nafasi ya Sam Allardyce ambapo tangia kuichukua timu hiyo amekuwa na wakati bora wa kufika hatua nzuri kwenye mashindano mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live