Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Southgate mambo yanazidi kuiva Man United

Southgate Uingereza Southgate mambo yanazidi kuiva Man United

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gareth Southgate amedaiwa kumbwaga Graham Potter kwenye mchakamchaka wa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kwenda kudaka dili la kuinoa Manchester United msimu ujao.

Kocha wa zamani wa Chelsea, Potter amekuwa kwenye mipango ya tajiri mpya wa Man United, Sir Jim Ratcliffe endapo kama ataamua kumfuta kazi Erik ten Hag.

Lakini, kocha wa England, Southgate wiki iliyopita alisema ameweka kando mpango wa kusaini mkataba mpya kwenye kikosi cha Three Lions hadi hapo baada ya fainali za Euro 2024 zitakapokwisha.

Tajiri Ratcliffe, ambaye anasimamia masuala ya soka kwenye kikosi hicho alisema: “Tukipata watu sahihi kwenye boksi, matokeo yatapatikana.”

Potter alifanya kazi kwa karibu sana na mkurugenzi wa michezo ajaye Man United, Dan Ashworth walipokuwa Brighton, lakini Southgate, naye alifanya kazi na bosi huyo kwenye chama cha soka.

Ripoti zinadai kwamba Sir Jim sasa anamtazama kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 kama chaguo la kwanza la kwenda kuchukua mikoba ya Ten Hag, aliyekalia kuti kavu Old Trafford.

Man United imekuwa na kiwango kinachopanda na kushuka kama homa za vipindi chini ya Ten Hag. Timu hiyo ilikomea hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku mabao iliyofunga 39 ni sawa nay ale iliyofungwa 39 kwenye msimamo wa EPL. Mkataba wa Southgate na England unafika tamati Desemba mwaka huu.

Na Ratcliffe anaamini atamrudisha tena kwenye soka la klabu baada ya kuinoa kwa miaka mitatu Middlesbrough hadi mwaka 2009. Hata hivyo, kumpata Southgate mwisho wa msimu Ratcliffe atalazimika kulipa fidia ya Pauni 800,000, huku akitaka kumwondoa Ten Hag, anapaswa kulipa fidia Pauni 10 milioni.

Lakini, Potter hana kazi na hahitaji kulipiwa fidia yoyote ili kunasa huduma yake. Kazi kwa Ratcliffe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: