Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Southgate ashauriwa kubaki na England

Skysports Southgate Football 5442191 1536x864 Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wa England na mashabiki wamemuomba Gareth Southgate asiachie ngazi baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia hatua ya rabo fainali dhidi ya Ufaransa.

Kocha huyo amewasili England akitokea Qatar lakini bado hajafanya maamuzi kuhusu hatima yake kama ataendelea kuinoa timu hiyo. Lakini mastaa wa timu hiyo akiwemo Declan Rice, Kyle Walker, Jude Bellingham, Harry Maguire na Kevin Trippier.

Kampeni ya kumsapoti Southgate imeanza kwani mastaa hao pamoja na benchi zima la ufundi England wanaamini kocha huyo anastahili kukiongoza kikosi kuelekea michuano ya Euro yatakayoanza kufanyika mwaka 2024, huko Ujerumani.

Naye kipa wa zamani wa England, Peter Shilton anaamini Southgate ndio kocha peke mwenye nafasi kubwa ya kuipa ubingwa taifa hilo kwenye michuano mabalimbali ya kimataifa.

“Southgate anastahli kubaki, tuna kikosi kikubwa cenye uwezo wa kubeba kombe, yajayo yanafurahisha, muhimu tuwe na imani tu safari bado ni ndefu," alisema mkongwe huyo.

Kocha wa zamani wa England, Sam Allardyce naye ameunga mkono hoja ya kumsapoti Southgate "Nitashangaa sana kama ataacha kazi, sijaona kocha mwingine zaidi yake, kila mtu anapenda kufanya kazi na Southgate kwasababu ni kocha mzuri,".

Beki wa zamani wa Man United na England, Gary Neville naye ameweka wazi hisia zake akisisitiza Southgate ndio mtu sahihi wa kuliendelezaa gurudumu la mafanikio.

"Southgate abaki tu kwa miaka mingine zaidi, haijalishi kama atakuwa kocha ama kiongozi wa Chama cha soka FA siku za usoni," aliandika Neville kupitia akaunti yake ya Twitter.

England imeshindwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa, lakini Waingereza wanaamini ipo siku Southgate ataipatia mafanikio timu yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live