Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Southgate:Najitafakari kujiuzulu

Gareth Southgatee Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amesema atafanya tathmini ya namna ambavyo fainali za Kombe la Dunia Qatar zimeenda sambamba na Chama cha Kandanda England FA kujua hatima ya kusalia ndani ya kikosi cha "Three Lions".

Southgate amesema hayo baada ya kuulizwa kama yuko tayari kuachia kiti cha ukocha kufuatia kupoteza na kutolewa na Ufaransa katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022 kwa kichapo cha bao 2-1.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alianza kuinoa England mwaka 2016 ambapo mkataba wake ni mpaka Euro 2024.

“Haya mashindano tumetoka kwa mengi, nahitaji muda wa kutafakari kama ambavyo nilifanya baada ya michuano mingine”.

Kwenye kipindi hicho cha takribani miaka saba, Southgate hajashinda taji kubwa lolote lakini amefika hatua nzuri kwenye mashindano makubwa mathalani kufika nusu fainali ya WC 2018 kisha kufika fainali Euro 2020.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live