Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Southampton waing'ang'ania Man United, Casemiro ala umeme

Casemiro Man United Red Card Southampton 031223.jpeg Southampton waing'ang'ania Man United, Casemiro ala umeme

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kusema maiti yamng’ang’ania muoshaji, hiyo ni baada ya kibonde wa Ligi Kuu England Southampton kuvuna alama moja muhimu ugenini kwa Manchester United kwa sare tasa iliyopatikana dimba la Old Trafford.

United wakiwa kwenye ubora mzuri wa mchezo walijikuta wakipokea tukio la kutotegemewa kufuatia kiungo mkabaji wa kimataifa wa Brazil Casemiro kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana ungwe ya kwanza kwa Carlos Alcaraz.

Baada ya kadi hiyo, Manchester United waligeuka kuwa wanyonge na muda mwingi wa mchezo wakatumia kutafuta mpira.

Kwa matokeo hayo, Manchester United inabakia nafasi ya tatu na Southampton inaendelea kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live