Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Soon' tutasikia wametua CAS - Luambano

Morrison Okwa 'Soon' tutasikia wametua CAS - Luambano

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa michezo wa Clouds Media, Alex Luambano amesema kuwa msimu huu timu nyingi nchini zimewaondoa baadhi ya wachezaji wake wengi hivyo huenda wapo walioondolewa kimakosa na wanaweza kwenda CAS kudai haki zao.

Timu karibu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara zimewafungasha virago baadhi ya wachezaji wao kutokana na viwango vyao kutoridhisha.

“Klabu zetu zinaacha wachezaji wengi kuliko zinaowauza, hadi sasa hivi unakuta timu imecha wachezaji nane [8] hadi tisa [9], nilitegemea kuona wameuza saba [7] wameacha wawili [2] au watatu [3].

“Huku wkenye kuacha ndani yake kuna hasara, kuna wanaoachwa kwa kuvunjiwa mikataba, kwa hiyo kuna makubaliano ya kuwalipa wachezaji wenye mikataba ili klabu iwaache!

“Kuna ‘THANK YOU’ ningine zina gharama, sasa hivi kuko kimya baada ya muda utasikia kesi zipo FIFA, watu wanaambiwa hakuna kusajili hadi mchezaji alipwe.

“Vipngozi wa klabu wanapotoa hesabu za mapato na matumizi wanatakiwa waseme pia mapato yatokanayo na mauzo ya wachezaji na malipo kwa wachezaji walioachwa, lakini hawasemi!

“Wakati watu wanakwenda mbele kwenye biashara ya kuuza wachezaji, sisi tunarudi nyuma!," amesema Alex Luambano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live