Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Son ajilaumu kufukuzwa kwa Antonio Conte

Son X Conte Nyota wa Tottenham Hotspurs, Son Heung-min

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Tottenham Hotspurs, Son Heung-min amejibebesha lawama nyingi baada ya Antonio Conte kufukuzwa kazi na anaaamini yeye ndiye chanzo.

Fowadi huyo wa Kimataifa wa Korea Kusini amekuwa na wakati mgumu msimu huu baada ya kubeba kiatu cha mfungaji bora msimu wa 2021-2022, mpaka sasa amefunga mabao 10 katika mechi 37 alizocheza katika mashindano yote.

Son amekiri endapo kiwango chake kingekuwa bora angemsaidia Conte kuibeba Tottenham ambayo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

“Nimejisikia vibaya kwa ajili yake, tulikuwa na ndoto nyingi pamoja, namshukuru kwa kila kitu, sijajua kama wachezaji wengine wanamfikiria, kwa upande wangu nimesikitika, nadhani nimemuangusha kwa kiasi fulani, sikumsaidia kwa sababau sikupambana nadhani nimehusika katika haya yote,” alisema Son.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: