Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Solskjaer kuagwa Old Trafford wiki hii

0 Ole Gunnar Solskjaer Aliekuwa meneja wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya miaka 3 ya kuingoza Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameondolewa klabuni hapo. Old Trafford kumuaga Ole wiki hii.

Solskjaer alitimuliwa United baada ya matokeo mbaya kwenye michezo 5 kati ya 7. Kibaya zaidi, wakiwa Old Trafford, United wamepoteza michezo dhidi ya Liverpool, Man City, Aston Villa na West Ham.

Yote kwa yote, kufuatia kupokea kipigo cha magoli 4-1 dhidi ya Watford kule Vincage Road, mashabiki wa United hawakupata nafasi ya kumuaga Ole na sasa, sehemu ya mashabiki wao, wamepanga kumuaga kocha huyo kwa heshima anayostahili.

Ukiachana na matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu huu, Ole anabaki na heshima yake kama miongoni mwa wachezaji magwiji wa United. Heshima hii pia, inaendana sambamba na kazi nzuri aliyoifanya kwa muda wote aliokuwa kocha wa United.

Kwa maana hiyo, mashabiki wanaotumia upande wa Stretford End, wamepanga kuzungusha bendera yenye picha na ujumbe kwa Ole Gunnar Solskjaer kama sehemu ya kumuaga kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live