Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#SokaTBT: Terry apasuka kichwa, aendelea kukichafua

Terry Butcher England Sweden 1 Terry

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wa michezo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia kati ya Uingereza na Sweden mwaka 1989, beki wa Uingereza, Terry Butcher aligonganana na straika wa Sweden, Johnny Ekstrom na kuvunjika kichwa.

Tukio hilo lilitokea katika kipindi cha kwanza cha mzezo huo huku majeraha hayo makubwa yakimwacha Terry akivuja damu nyingi na jezi yake kutapakaa damu mwili mzima.

Baada ya kuopkea matibabu na kufungwa bandeji, aliendelea na mchezo huo. Mpaka dakika ya 90, jezi ya Butcher iliyokuwa nyeupe ilikuwa imechafuka damu mithili ya mbuzi aliyechinjwa.

Lakini cha kushangaza, mechi ilimalizika kwa sare ya bila kufungana, sare ile ilikuwa faida kwa Uingereza kwani walifanikiwa kupenya kwenda michuano ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990 iliyofanyika nchini Italy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: