Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Slot aambiwa amng'ang'anie Salah

Slot Pict Slot aambiwa amng'ang'anie Salah

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Chris Sutton amemwambia kocha wa Liverpool, Arne Slot atatakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah anabaki.

Salah ambaye amebakisha miezi 10 katika mkataba wake, dirisha lililopita la majira ya kiangazi Al-Ittihad ya Saudi Arabia iliwasilishwa ofa ya Pauni 150 milioni kwenda Liverpool kwa ajili ya kumsajili na ikawa tayari kumpa mshahara unaofikia Pauni 100 milioni lakini ilikataliwa.

Licha ya ukweli Liverpool inaweza kupata ada kubwa ya uhamisho wa Salah ikiwa wataamua kumuuza dirisha hili, Sutton amesema Slot hapaswi kujaribiwa kutoa ruhusa ya kuuzwa Salah kwa sasa hata kama pesa zitakazopatikana zitatumika kufanya manunuzi ya wachezaji wengine.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Blackburn na Chelsea alisema Salah ni mchezaji muhimu sana kwa Liverpool na Slot anamhitaji sana kwa ajili kufanya vuzuri katika msimu wake wa kwanza.

"Ikiwa wewe ni Arne Slot, lazima utamhitaji na ili kufanya hivyo, utatakiwa kuhakikisha unambakisha Mohamed Salah kwa sababu ni mmoja wa wachezaji bora katika timu, ukiwa kocha unahitaji kupambana na kufanya vizuri katika msimu wako wa kwanza, viatu ambavyo Slot anajaribu kuvivaa vimeachwa na Jurgen Klopp, ni vikubwa na ngumu sana kuvivaa, ili kufanikisha hilo anatakiwa kuendelea kumshikilia Salah ili kupata nafasi ya kufanikiwa."

Salah ambaye amefunga mabao 211 na kutoa asisti 89 katika mechi 349 za michuano yote aliyochezea akiwa na Liverpool, kati ya hizo, mechi 250 ni za EPL na alifunga mabao 155, vile vile Ligi ya Mabingwa amefunga mabao 41 na kutoa asisti 14 katika mechi 64.

Mabosi wa Saudia wanataka kumsajili Salah kwa sababu amekuwa ya ubora wake na kibiashara na wanaamini kutua kwa fundi huyo kutasababisha kundi kubwa la mashabiki kutoka Misri na nyingine Afrika kuendelea kufuatilia zaidi ligi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live