Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu ni waziri wa raha ya soka, ni mtu hatari - Ally Kamwe

Skudu Makudubela Skudu Makudubela.

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa usajili walioufanya wa kumleta winga machahari Skudu Makudubela si wa kitoto.

Kamwe amesema kuwa mchezaji huyo ni hatari na mwenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira hivyo Wananchi wajiandae kupata ushindi na burudani ya soka ndani yake.

“Tuliwambia mapema kuwa pale Afrika Kusini tumesajili mshambuliaji wa viwango. Hili liwekeni sawa tumemchukua mtu hatari sana Mfalme wa Amapiano nikisema nimwelezee nitakupotezea muda wako.

"Kibwana Shomari kanipigia simu usiku kaniambia afadhali watu waone maana siku ile alikuwa anamgeuza Kibwana anahamia kwa Dickson Job, lakini ukumbuke hawa ni mabeki wakubwa, lakini jamaa aliwatesa.

"Kiu ya wananchi kuhusu atakayevaa jezi namba sita wa yanga umemalizika ipasavyo, mmeona Wananchi walivyompokea kwa vibe Makudubela, Skudu Master, Technician, ball player, ball dancer.

"Hii inaonyesha msimu ujao sio tu tutashinda mataji bali tutapata raha ya mpira, huyu ni waziri anayemiliki wizara mpya kwenye soka, wizara ya raha," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: