Winga wa Klabu ya Yanga, Skudu Makudubela amerea nchini Tanzania akitokea kwao Afrika Kusini alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu baada ya kuumia kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
Skudu amerejea na mkewe usiku wa kuamkia leo na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa Yanga, mashabiki na wanahabari karika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam huku akiahidi kuendeleza mazuri na kuisaidia timu yake katika malengo ambayo imejipangia msimu huu.
"Ninafuraha kubwa kurejea tena klabuni baada ya kutoka lwenye majeraha niliyoyapata hapo awali, nilikuwa kwenye matibabu na daktari wangu alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na daktari wa klabu kuhusu maendeleo, nadhani mpaka Jumatatu ripoti ya daktari itakuwa imetoka na kujua sasa nini kinaendelea.
"Nilipokuwa nyumbani nilikuwa naifuatilia timu yangu, hususani mechi ya Ligi dhidi ya KMC, wachezaji wote walijituma sana, kwakweli ni jambo la kumshukuru Mungu tulipata matokeo.
"Benchi la ufundi linafanya kazi vizuri, rotation ya wachezaji kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi na hii inasaidia kulinda kipaji cha kila mchezaji ndani ya kikosi, nawapongeza walimu kwa hilo.
"Nimekuwa nikipokea meseji nyingi za mashabiki wakisema wanataka nirudi wamemiss kuniona dimbani, nawaambia nimerejea kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi, natamani nione tunampiga mwingine bao tano," amesema Skudu.