Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu anateswa na jina alilopewa

Skudu Makudubela Mbinu Mpt Skudu anateswa na jina alilopewa

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ilionekana ndio usajili mkubwa zaidi dirisha kubwa lililopita kwa Yanga. Maneno yakawa mengi sana mpaka Skudu mwenyewe katika kujipunguzia pressure akatoka hadharani na kukanusha kuwa yeye sio namba 6 anayeimbwa sana.

Mara paaaaap! Likaja jina la Waziri wa Raha, wapinzani wa Yanga wakatahadhalishwa kuwa amekuja mtu wa kuwasulubu kwa chenga za manyanyaso, mabeki wa timu maneno yakawajaa,Skudu mwenyewe maneno yakamjaa ndio maana hata kwenye kilele cha wiki ya wananchi akaingia kiburudani zaidi kuliko kazi.

Mechi ya kwanza ambayo ndio alitakiwa kuanza kuweka alama mioyoni mwa wanayanga akacheza dakika saba tu na shughuli yake ikaishia hapo, tangia hapo hata alipopona hakuamika tena,akaanza kutazamika kama mchekeshaji au mburudishaji kuliko shujaa wa timu.

Dakika zake zimekuwa ni mbili au tatu ,hapatiwi nafasi ya kuonesha alichonacho na hakuna anayehoji kwa sababu ya jina baya tulilompa. Dakika chache anazopewa mimi naona anakitu anachotaka kutuonesha lakini kipenga cha mwisho kimekuwa kinamsaliti.

Ninaposikia leo yuko mbioni kuachwa ninaishia tu kujiuliza ,ni lini alipewa nafasi ya kuonesha kile kilichowafanya Yanga wamlete kwa mbwembwe nyingi? Kuna mawili, walileta mchezaji bomu au ni mchezaji mzuri aliyenyimwa nafasi ya kuonesha kipaji chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live