Staa wa kwanza raia wa Afrika Kusini kucheza Ligi Kuu Tanzania, Mahlatse Makudebela ‘Skudu’, amesema anataka kuwaona Simba ili afahamu ubora wao.
Staa wa kwanza raia wa Afrika Kusini kucheza Ligi Kuu Tanzania, Mahlatse Makudebela ‘Skudu’, amesema anataka kuwaona Simba ili afahamu ubora wao. “Nasubiri kuwaona Simba ili nijue wana ubora kiasi gani, lakini kwa ujumla lazima nikuhakikishie kuwa tuna timu bora. Ni kazi kubwa kupata namba hapa kwani wachezaji wengi wako vizuri na wanahitaji nafasi ya kucheza, hivyo mtihani mkubwa ni kuonyesha uwezo kwenye kila mchezo,” alisema staa huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Marumo.