Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu amefikia matarajio au amefeli?

Skudu Makudubela Vvvv.jpeg Skudu Makudubela.

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wa dirisha kubwa la msajili katika dirisha hili la usajili mchezaji ambaye alitikisa au usajili wake ulifatiliwa zaidi ni huyu jezi namba sita (6) Skudu Makudubela maana kwa mujibu wa Msemaji wa Yanga Ally Kamwe Alisema Huyu mchezaji akayevaa jezi namba sita hajawahi kutokea nchi hii .

Katika mechi za ligi mpaka Sasa ambazo Yanga amecheza ni 13 wakiwa wanashikaa nafasi ya pili na point tuanze kuangalia mchango wa huyu mchezaji ambaye kwa upande wa Yanga ulitajwa kama usajili Bora zaidi kuwahi kutokea kwanza tunaona amekuwa hapati sana nafasi ya kuanza katika kikosi Cha kwanza amekuwa akioewa dakika chache katika ligi mpaka mechi za ligi ya Mabingwa.

Ukiangalia uwezo na kiwango chake bado ni mchezaji wa kawaida hata ukiangalia mpaka hapa ligi ilipofikia unaweza kusema amefeli maana ukitazama katika orodha ya Wafungaji Bora hayupo wachezaji waliotoa pasi nyingi za Magoli hayupo maanake Skudu amefeli ameshindwa kuisaidia timu yake mpaka Sasa anagoli Moja tu katika mechi zote za mashindano alizocheza.

Skudu amefeli alitambulishwa kwa mbwembwe kuliko mchezaji yoyote ambaye amesajiliwa msimu huu lakini wenzake wakina Max Nzengeli pamoja na Kouassi Ottoula Yao pamoja na Pacome Kila mmoja amefanya kazi kubwa ya kuiweka Yanga katika ubora ndiyo maana wameweza kuingia makundi baada ya miaka 25 lakini katika ligi ya Mabingwa Pacome amefunga mabao muhimu katika ligi Max Nzengeli amefunga Magoli tofauti ya yeye Skudu kupata namba tu imekuwa shida .

NB: Skudu amefeli tofauti na mbwembwe za usajili wake

Chanzo: www.tanzaniaweb.live