Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu afunguka alivyoona simu ya Eng. Hersi

Skudu Makudubela.jpeg Skudu afunguka alivyoona simu ya Eng. Hersi

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela Manoka 'Skudu' raia wa Afrika Kusini kwa mara ya kwanza amefunguka namna alivyopigiwa simu na Rais wa yanga, Eng. Hersi Said akimtaka ajiunge na miamba hao wa soka.

Skudo aliyekuwa akikipiga Marumo Gallants amesema kuwa ameheshimishwa kupewa jezi hiyo na ni deni kwake kuitendea haki ili kuwafurahisha mashabiki wa Yanga kwa kusaidiana na wachezaji wenzake kuiletea mafanikio zaidi klabu hiyo.

"Wakati Injinia Hersi ananipigia nilikuwa nakaribia kusaini mkataba na klabu moja kubwa nchini Afrika Kusini, lakini nilipoona simu ya rais nikasema nani anaweza kukataa kupokea simu ya Rais? Kwa hiyo nilipokea na tukazungumza. Ninafurahi kujiunga na klabu kubwa Afrika Mashariki.

"Mafanikio makubwa ya Yanga na malengo yake ndiyo vimenishawishi kujiunga na klabu hii. Ukiwa mchezaji bora unahitaji kuitumikia timu bora, kwa hiyo Yanga waliponipigia nilisema siwezi kukataa.

"Nimetazama historia ya klabu, malengo ya timu, mafanikio ambayo timu imepata kwenye misimu iliyopita, kubeba mataji yote ya ndani, kufika fainali ya CAF, ni sehemu ya mambo makuu yaliyonishawishi. Mimi ni mchezaji mkubwa lazima niwe kwenye timu kubwa.

"Wakati tunakuja kucheza hapa mechi ya kwanza nikiwa na Marumo ilituchanganya, tulikuta mashabiki wengi wenye vibe, presha ikawa kubwa upande wetu, haijawahi kutokea, Afrika Kusini kuna mashabiki lakini ni timu kubwa za Orlando na Kaizer zenye mashabiki wengi kama hapa na hawana vibe kubwa kama walilonalo mashabiki wa Tanzania.

"Ninawaomba mashabiki tuungane, tupambane tena msimu huu ili kubakisha mataji yetu ya ndani tuliyoshinda msimu uliopita na kufanya vizuri zaidi kimataifa. Siwezi kusubiri kuingia uwanjani na kuwapa furaha mnayoitarajia kutoka kwangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu, asanteni wananchi," amesema Skudu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: