Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu: Yanga wameniheshimisha kunipa namba 6

Skudu Ews Mahlatse Makudubela Manoka 'Skudu'.

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela Manoka 'Skudu' raia wa Afrika Kusini kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu kupewa jezi namba 6 ndani ya kikosi hicho.

Skudo amesema kuwa ameheshimishwa kupewa jezi hiyo na ni deni kwake kuitendea haki ili kuwafurahisha mashabiki wa Yanga kwa kusaidiana na wachezaji wenzake kuiletea mafanikio zaidi klabu hiyo.

"Imekuwa ni furaha kuliwakilisha Taifa la Kijani na Njano, na ninadhani mapokezi yalikuwa mazuri sana, ninajisikia nipo nyumbani tayari, asanteni sana Wananchi.

"Kwenye mitandao ya kijamii nilikuwa naona namba 6 ina-trend, lakini sikujua ni nini hasa. Nilianza kufuatilia kwenye kurasa za Yanga na Ally Kamwe, mashabiki wa Yanga wanaonekana walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kumjua mchezaji huyo, hii ilianza kukaa kichwani mwangu.

"Nimeheshimishwa sana kupewa jezi namba sita, Imani kubwa waliyo nayo juu yangu mpaka kunipa jezi hiyo ni kubwa sana, ninajua ni namba ngumu lakini nitaishi kulingana na matarajio ya klabu ili kufikia mafanikio yaliyolengwa.

"Ninawaomba mashabiki tuungane, tupambane tena msimu huu ili kubakisha mataji yetu ya ndani tuliyoshinda msimu uliopita na kufanya vizuri zaidi kimataifa.

"Siwezi kusubiri kuingia uwanjani na kuwapa furaha mnayoitarajia kutoka kwangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu, asanteni wananchi," amesema Skudu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live